
Shirika la Wapasionisti lilianzishwa na Mt. Paulo wa Msalaba mwaka 1720. Mwaka huu tunasherehekea Jubilei ya miaka 300 tangu kuanzishwa kwa shirika letu. Lengo la maadhimisho haya ni kueneza wito wa UTUME wetu wa kuwaunda watu kwa njia ya msukumo wa Mitume, Manabii na Mashahidi wa Upendo wa Kristo Msulibiwa.
Maneno matatu yanabeba ujumbe wetu:
- SHUKRANI: Tunawasifu na kuwashukuru ndugu zetu waliotutangulia, na ambao hadi sasa wamekuwa chanzo cha mtiririko mkubwa wa upendo. Tunawashukuru kwa sababu, kwa mchango wao, Shirika sasa limeenea katika nchi 60 ulimwenguni, na katika jumuia zaidi ya 400.
- UNABII: Tunaamini kwamba bado ni muhimu kutimiza mpango wa Mungu. Ni manabii wa kila siku tunaotumia Neno la Mungu na Matumaini yetu kama bendera yetu. Ni manabii tunaokemea yale yasiyofaa na kupendekeza suluhisho lililo bora zaidi. Tunaukumbuka upendo wa Mungu anayependa MWANGA uondoe kila kivuli. Katika ulimwengu wetu huu, watu wengi wanahitaji sana wanahitaji maneno ya upendo, wema na faraja.
- MATUMAINI: Tunasukumwa kujenga matumaini mapya. Tunakuwa na mtazamo chanya juu ya maisha unaotokana na tumaini lisiloshindwa kwa Kristo Msulibiwa.