Vocations Director

Rev. Br. Ludovick Said C.P.
Vocations Director
WATAWA WA SHIRIKA LA MATESO YA YESU KRISTO NI NANI?
· Watawa wa Shirika la Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo wanaishi na kufuata kanuni za mwanzilishi wa Shirika Mtakatifu Paulo wa Msalaba.
· Tunaishi maisha yetu katika jumuiya tukitafakari, tukifuata na kutangaza mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.
“...katika kila aina ya mateso ya binadamu kuna msalaba wa Yesu...yeyote ampendaye Yesu hatafuti chochote isipokuwa kushiriki mateso yake...” (Paulo wa Msalaba)
KARAMA NA LENGO
· Kumtangaza Kristo Msulubiwa kwa Mapendo kwa Wasulubiwa wa wakati wetu na kudhihirisha kwamba Kristo aliteswa na kufa Msalabani kwa ajili ya wokovu wetu.
· Watawa wa Shirika la Mateso ya Kristo wanatekeleza karama ya mwanzilishi katika:
§ Maisha ya Jumuiya
§ Mahubiri - uinjilishaji wa kina na mafungo ya kiroho
§ Kazi za kitume
§ Umisionari – kwenda kumtangaza Kristo popote
§ Misioni - katika parokia
§ Maendeleo ya jamii
WITO WA KIPASIONISTI
· Wito wa kipasionisti waweza kutekelezwa katika Upadre na Ubruda.
o Upadre: Kujitolea kwa Mungu na kuwatumikia ndugu katika kazi za Kikuhani na za kawaida.
o Ubruda: Kujitolea kwa Mungu na kuwatumikia ndugu katika kazi za katekesi na za kawaida.
WATAWA WAPASIONISTI
· Wito katika Shirika letu ni kuishi masharti ya Injili kwa dhati, kwa njia ya nadhiri za kitawa:
1. Umaskini
2. Useja
3. Utii
4. Kutangaza Mateso ya Kristo na Kuishi Maisha ya Jumuiya
· Ni kujitolea kuwa mali ya Mungu na Mtumishi wa wote, kuishi kijumuiya na kujikita kwenye Utume.
· Kumfuata Kristo katika njia yake ya Mateso na Ufufuko kupitia Utume kwa lengo la kujitakatifuza na kuwatakatifuza wengine.
Ewe kijana, je, umetambua wito wako?
Je, upo tayari kuitikia wito huo wa Mungu?
SIFA ZA MWOMBAJI:
· Awe amehitimu elimu ya Sekondari, Kidato cha sita na kufaulu vizuri au elimu ya Chuo kikuu.
WASILIANA NA:
MKURUGENZI WA MIITO
SHIRIKA LA MATESO YA YESU KRISTO
S.L.P. 990
DODOMA
Mobile: +255 755 849191 / +255 682 922383
Email: vocationsdirector@passioniststanzania.or.tz
Website: www.passioniststanzania.or.tz
Download our Brochure